RAIS TFF:- FIFA KUFANYA MKUTANO DAR ES SALAAM FEB 22 - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday, 3 January 2018

RAIS TFF:- FIFA KUFANYA MKUTANO DAR ES SALAAM FEB 22


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia, akizungumza na waandishi wa habari.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepata uenyeji wa mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) unaotarajiwa kufanyika Februari 22 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere ulioko eneo la Posta jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika mkutano wake na waandishi wa habari, Rais wa TFF, Walace Karia, amesema ni faraja kubwa kwa Tanzania na shirikisho lake kupata uenyeji huo ambao ni ugeni mkubwa na utaleta fursa ya kipekee kwa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Ameongeza kwamba mkutano huo utazikutanisha nchi 19 ambapo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, atahudhuria.

Alizitaja nchi zitakazoshiriki mkutano huo kuwa ni pamoja na Tanzania, nchi za Arabuni, Afrika na za Bara la Amerika.

No comments:

Post a Comment