RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amesema kitendo
kilichofanyika cha kutoa msamaha kwa wafungwa 8,158, ikiwemo familia ya
Nguza Viking siyo yeye aliyofanya bali ni Mungu ndiye aliyefanya na
ndiyo anapaswa kupewa shukrani.
Rais Magufuli amesema hayo leo baada ya kutembelewa na familia ya
Mzee Nguza Viking ilipomtembelea Ikulu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa
kile alichokifanya Disemba 9, 2017 kwa kutoa msamaha uliowatoa kifunguni
walikokuwa wakitumikia kifungo cha maisha.
“Mimi sikutegemea kama mtakuja kuniona na kunishukuru,
niliyoyafanya haya si mimi, bali ni mipango ya mwenyezi Mungu, shukurani
nyingi zimuendee Mwenyezi Mungu aliyetuumba na ndiyo mwenye jukumu
kubwa la kusamehe, binadamu hatuwezi tukasimama badala ya Mwenyezi
Mungu,” alisema Rais Magufuli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameisisitiza familia ya Nguza kuishi
maisha mapya ya kumtukuza Mungu kwani maisha yanapita, yana kuanguka,
kusimama hivyo wamtegee yeye (Mungu). na kwamba mategemeo yake sasa ni
kuona wanafanya kazi na magitaa yananguruma .
Disemba 09, 2017 kwenye sherehe za Muungano wa Tanzania, Rais
Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,158 ikiwemo familia ya Nguza
Viking.
No comments:
Post a Comment