MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye (CCM),
amesema kuwa hana mpango wa kuhamia chama chochote cha upinzani na
ataendelea kubaki ndani ya CCM. Alisema
hawezi kufanya uamuzi wa kuhamia katika vyama vya upinzani , huku
akidai magari ya upinzani kwa sasa yanazidi kuzama na haijulikani
yataibuka lini.
Kauli hiyo aliitoa mjini Songea
wakati akimnadi mgombea Ubunge wa Songea kupitia CCM, DK. Damas Ndumbaro
katika mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Bombambili mjini hapa. Nape
ambaye pia aliwahi kuwa katibu Mwnezi wa CCM, alisema kama kuna watu
walidhani atakihama chama tawala CCM na kujiunga na upinzani wasahau.
Alisema matatizo ya chama humalizwa ndani ya chama na si kukihama kama walivyofanya wanachama wengine
waliokimbia ndani ya CCM.
“Naikubali serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Jemedari, DK. John Magufuli, Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa. Ni serikali yenye
viongozi imara na mimi naapa kufia CCM na sivinginevyo.
“Nasikia maneno maneno kutoka kwa
baadhi ya watu wakisema Nape anataka kuhamia upinzani jambo ambalo siyo
la kweli kuanzia leo watu hao waondokane na mawazo hayo,” alisema Nape.
No comments:
Post a Comment