Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda leo amemsaidia Mjane Bi.
Benadetha Rwendela aliyedhulumiwa Nyumba yake Plot No. 239 Block B
Kunduchi Beach kwa kupigwa mnada na madalali kutoka kampuni ya Nkanya
Ltd kinyume na taratibu.
Baada ya RC Makonda kuona taarifa hizo kwenye baadhi ya Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii alimwita mjane huyo Ofisini kwake kisha kumkutanisha na Wanasheria wa Mkoa na kubaini utapeli mkubwa uliotumika kuuza nyumba hiyo kutokana na watu kufoji nyaraka ikiwemo Sahihi ya Mwenyekiti wa mtaa huku nyumba hiyo ikiwa na zuio la Mahakama.
Aidha imebainika kuwa hati za nyumba hiyo zilifojiwa kisha kutumika kuchukuwa mkopo wa Shilingi Billion moja pasipo mmiliki wa nyumba kujua kinachoendelea.
Kutokana na hilo RC Makonda ameagiza Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa kuwakamata matapeli waliohusika pamoja kuagiza kusimamishwa mnada huo kwakuwa ni batili huku akimsihi Mama Mjane kuishi kwa amani kwenye nyumba yake.
Kwa upande wake mjane huyo Bi. Benadetha Rwendela ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwajali Wananchi wake na kuwasaidia pale wanapopata matatizo huku akimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua RC Makonda.

No comments:
Post a Comment