KLABU ya Liverpool imewakodia ndege mastaa wake wawili, Sadio Mane na
Mohamed Salah ambao wanakwenda kushiriki utoaji wa Tuzo za Mchezaji
Bora wa Afrika.
Wachezaji hao wanatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo keshokutwa Alhamisi na kutarajiwa kurejea usiku huohuo nchini England.
Liverpool wametoa taarifa kuwa wachezaji hao watakodiwa ndege na
ilikwenda nchini Ghana kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za utoaji wa tuzo
hizo ambazo wote wawili wanashiriki.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema kuwa anaamini wachezaji hao
wanaweza kwenda na kurejea England kucheza mchezo wa Kombe la FA, dhidi
ya Everton, Ijumaa.
“Wataondoka hapa asubuhi na watarejea mara tu baada ya tuzo hizo
kumalizika, hawatakuwa na muda wa kupoteza kwa kuwa wana mchezo Ijumaa,”
ilisema taarifa kutoka Liverpool.
“Tumeandaa kila kitu vizuri, tuna wachezaji wawili kati ya watatu
ambao wanawania tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Afrika, lazima tuwaonyeshe
heshima."
“Sisi kwetu kila kitu kipo kwenye mpangilio mzuri sana na wa heshima
kuwa kila mmoja ambaye tunafanya naye kazi,” alisema kocha wa Liverpool,
Juggen Klopp.
Salah bado anasumbuliwa na majeraha ya nyonga ambayo yalimfanya
aukose mchezo wa juzi dhidi ya Burnley na kocha huyo amesema kuwa kama
atakuwa hawajapona hadi Ijumaa basi hatacheza mchezo dhidi ya Everton.
No comments:
Post a Comment