MBUNGE wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika
(TLS), Tundu Lissu ambaye sasa Kenya akiendelea na matibabu kufuatia
kupigwa risasi Septemba 7, 2017 amefunguka juu ya viongozi ambao
wanakisaliti CHADEMA na kusema jambo hilo lisiwatishe bali wao waendelee
na kazi yao.
Tundu Lissu aliyasema hayo jana alipoonana Mwenyekiti Mpya wa
Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye
alimtembelea Mhe Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali
“Ndugu zangu Mhe Lissu ameweza kunieleza mambo mengi sana na
binafsi naamini ameniagiza kwa niaba ya Baraza la Vijana na
tutayetekeleza kwa maslahi mapana ya nchi na chama chetu, hajasita
kuniambia kwamba hali ya siasa yetu ndani ya nchi yetu kwa biashara
inayoendelea kununua Viongozi uchwara na wenye tamaa wa chama chetu,
amesema tusipate hofu CHADEMA hatujaanza kusalitiwa leo na hao
wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kwani mbona Yesu aliwahi kusalitiwa
tena na mwanafunzi wake na hakuacha kazi yake” aliandika Ole Sosopi.
Aidha Sosopi aliendelea kusema kuwa Tundu Lissu amemweleza kuwa
hata watu ambao waliwahi kuisaliti CHADEMA kipindi cha nyuma hawajapata
mafanikio yoyote katika maisha yao
“Wanaotusaliti hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao,
tusikate tamaa mapambano yaendelee. Mwisho kabisa Mhe. Lissu ametuma
salamu nyingi kwa Watanzania wote wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea,
ameendelea kuwasihi waendelee kumchangia na kumuombea, maana Bunge na
serikali wamekataa kabisa kumtibia ili hali kwa mujibu wa sheria ni haki
yake,” alisema Ole Sosopi.
No comments:
Post a Comment