MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu kesi ya aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani
Madabida na wenzake watano wanaokabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi
kuhamishiwa Mahakama ya Mafisadi kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na
uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Madabida na wenzake wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwamo
kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ‘ ARV’s ‘ na
kusababisha hasara ya Sh.Mil 148 ambayo ipo chini ya bilioni moja ambapo
walifunguliwa kesi hiyo mpya namba 80 ya 2017, baada ya mahakama
kuwafutia kesi kama hiyo iliyofunguliwa mwaka 2014.
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ni Seif Shamte (mkurugenzi wa
uendeshaji), Simon Msoffe (meneja masoko) na Fatma Shango (mhasibu
msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd, Sadick Materu na
Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa. ambapo washtakiwa
hao wanadaiwa kuisambazia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kopo 4476 za ARV.
Pia washtakiwa wanadaiwa kujipatia Dola za Marekani 98,506.08 (sawa
na Sh 148,350,156 za Tanzania kwa udanganyifu baada ya kuonyesha kwamba
fedha hizo ni malipo ya makopo 12252 ya dawa hizo za ARV’s.
Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa mbele ya hakimu Mkazi, Victoria Nongwa
na Wakili wa Serikali, Pius Hilla Wakati ambapo upande wa utetezi wa
watuhumiwa wanawakilishwa mawakili Denis Msafiri, Makaki Masatu na
Nehemiah Nkoko ambapo wakili wa utetezi, Msafiri alidai kuwa Mahakama ya
Kisutu inayo mamlaka ya kuisikiliza hiyo kwa sababu kiwango chake cha
fedha kipo chini ya Sh.1 bilioni.
No comments:
Post a Comment