TIMU
ya Singida United imeingizwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na
itakuwa Kundi A pamoja na Yanga SC, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya
Jan’gombe.
Kundi linabaki kuwa na timu za Simba, Azam FC, URA, Jamhuri na Mwenge baada ya kuondolewa kwa Taifa ya Jang’ombe iliyohamishiwa Kundi B ambako imeondolewa Shaba.
Michuano ya Mapinduzi itaanza kesho kwa mechi kati ya Mlandege na JKU Saa 8:30 mchana, kabla ya Jamhuri kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni na Zimamoto kupepetana na Taifa ya Jan’gombe Saa 2:15 usiku, zote zikichezwa Uwanja wa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza mashindano Jumapili kwa kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni kabla ya Jamhuri kumenyana na URA Saa 2:15 usiku, wakati vigogo Simba na Simba wao wataanza mashindano Janauri 2, 2018.
Simba wataanza na Mwenge Saa 10:30 jioni wakati Saa 2:15 usiku Yanga watapepetana na Mlandege, mechi ambazo zitatanguliwa na mchezo kati ya Singida United na Zimamoto.
Azam watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi zake za Kundi A.
Simba watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
Yanga wao watarudi uwanjani Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.
Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.

No comments:
Post a Comment