Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto
Kabwe ametoa wito kuwa, Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa
Umma liwe linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua mali, madeni
na maslahi ya viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo
sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na
Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipasavyo.
Zitto amewasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ili kuweka vifungu
vitakavyolazimisha Bunge kuweka wazi muhtasari wa matamko ya Mali na
Madeni ya Wabunge (wakiwemo Waziri Mkuu na Mawaziri).



No comments:
Post a Comment