RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Amri Jeshi Mkuu, ametangaza msamaha kwa Nguza Viking maarufu kama
Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza (Papii Kocha) ambao waliofungwa maisha
katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kutaka waachiwe huru
mara moja kutoka gerezani.
“Tanzania tuna jumla ya wafungwa 39,000
ambapo wanaume ni 37,000 na wanawake 2,000. Wafungwa waliohukumiwa
wako 522 kati yao wanaume ni 503 na wanawake ni 19. Nimeamua kusamehe
wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu wafungwa 1828 watatoka leo.
“Mfano wa watu niliowasamehe ni Mzee
Mganga Matonya mwenye umri wa miaka 85 amekaa Gerezani miaka 37 na miaka
7 ya kukaa mahabusu. Nimeamua kusaheme familia ya Nguza Viking jina
lingine anaitwa Babu Seya na Ndugu Johnson Nguza ama Papii Kocha".
“Nimeamua kuwasamehe wafungwa 61
waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Lakini katika kuchunguzwa kwingi wapo
wafungwa ambao wametubu dhambi zao, wamekiri makosa yao kwelikweli,”
alisema Magufuli.
Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu
walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa
Shule ya Msingi Mashujaa, mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.
Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa
lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha
maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru
Mbangu na Chichi Februari 2010.
No comments:
Post a Comment