NBA Msimu 2017/18 waanza Kupamba moto - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday, 11 October 2017

NBA Msimu 2017/18 waanza Kupamba moto


  LIGI ya NBA inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa timu zote kuonyesha umwamba wao uwanjani, huku kila timu ikitaka kuhakikisha msimu huu inatwaa ubingwa.
Tayari timu zote zimeshaanza maandalizi ya msimu wa ligi hiyo na zingine zimeshaonyesha dalili za kuwa zinaweza kufanya vizuri mwaka huu.

Jumapili iliyopita kulikuwa na michezo nane ya maandalizi ya msimu, yaani (pre season), ambazo kati ya mechi zote hizo zilikuwa na matokeo ya kushangaza sana.
Spurs yawash-angaza Nuggets
Vijana wa San Antonio Spurs, walionyesha ubora wao Jumapili na kuanza kuwafanya mashabiki wawaweke kwenye kundi la timu zinazo-weza kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kufan-ikiwa kuwa-chapa Denver Nuggets, kwa pointi 122-100.
LaMa-rcus Aldridge, alikuwa bora kwenye mchezo huo baada ya kufanikiwa kufunga pointi 21, rebaundi tisa na kutoa pasi sita za pointi.
Bryn Forbes, naye hakuwa nyuma kwenye mchezo huo baada ya kufanya juhudi na kujikuta akipata pointi 20 kwenye mchezo huo.
Rudy Gay na Danny Green wote walifunga pointi 11 kila mmoja, huku Davis Bertans akimaliza mchezo huo kwa kuwa na pointi kumi.

Nikola Jokic, alikuwa shujaa kwa Nuggets kwa kuwafungia pointi 19, rebaundi saba na pasi nne za pointi kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi ya hali ya juu.
Will Barton alifunga pointi 16, Garry Harris akafunga 15 huku Paul Millsap, akifunga pointi 13, rebaundi saba, akitoa pasi tatu kwenye mchezo huo.

Warriors na Curry wakipiga China
Vijana wa Golden State Warriors juzi walifanikiwa kuwachapa Minnesota Timberwolves kwa pointi 142- 110, kwenye mchezo mkali uliopigwa Shanghai, China.
Stephen Curry, alionyesha kuwa anarejea tena msimu huu kwa moto baada ya kufanikiwa kufunga pointi 40 na kutoa pasi tisa.

Wakati yeye akifanya maajabu hayo na kushangiliwa na mashabiki wengi waliokuwa uwanjani hapo, Klay Thompson, alifunga pointi 28, huku staa wa msimu uliopita Kevin Durant akimaliza mchezo huo na pointi 22.
Andrew Wiggins, alikuwa shujaa kwenye kikosi chake cha Timberwolves alipomaliza mchezo huo kwa kufunga pointi 21.
Karl-Anthony Towns yeye alimaliza mchezo huo kwa kuwa na pointi 16, Jimmy Butler alifunga 15, Gorgui Dieng akafunga 11 na Jeff Teague akafunga 10.

Wizards yawachapa Cavaliers
Vijana wa Washington Wizards, juzi walionyesha kiwango cha juu walipopata ushindi wa pointi 102-94, dhidi ya Cleveland Cavaliers nchini Marekani.

Cavaliers walitumia wachezaji 11 tu kwenye mchezo huo, huku wakiwakosa mastaa wao kama LeBron James, Kevin Love, Tristan Thompson, JR Smith, Iman Shumpert na Derrick Rose.
Wizards walionekana kuonyesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo huku mastaa wao Jodie Meeks na Carrick Felix kila mmoja akifunga pointi 13, huku Bradley Beal akifunga pointi 11.

Jeff Green alionyesha kuwa bado anaweza kuisaidia timu yake msimu huu baada ya kuwafungia Cavs pointi 19.
Mchezaji huyo alipata shangwe nyingi sana kwenye robo ya pili ya mchezo huo kutokana na kufunga pointi muhimu sana kwenye mchezo huo.
John Holland alifunga pointi 14 wakati Kay Felder akifunga 12 na rebaundi 11.


No comments:

Post a Comment