MH MALIMA AFIKISHWA TENA LEO MAHAKAMANI - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 4 October 2017

MH MALIMA AFIKISHWA TENA LEO MAHAKAMANI


KESI ya Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na dereva wake, Ramadhan Mohammed, ya kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yao na kushambulia, imeahirishwa hadi Novemba Mosi mwaka huu.
Adam Malima akiwa katika Mahakama ya Kisutu leo.

KESI ya Naibu Waziri wa Fedha wa zamani, Adam Malima na dereva wake, Ramadhan Mohammed, ya kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yao na kushambulia, imeahirishwa hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Kesi hiyo iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirishwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama hiyo kuwa shahidi aliyetakiwa kutoa ushahidi hakupata mwaliko kwa wakati licha ya kuwepo kwa shahidi mwingine mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita, akisaidiana na Glory Mwenda, alidai Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na tayari walikuwa na shahidi Mwita Joseph, lakini kutokana na asili ya kesi hilo, aliyepaswa kutoa ushahidi alitakiwa kuwa Daktari Mchwempaka kabla ya Joseph.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Mwijage aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi mwaka huu itakapoendelea na ushahidi.

Katika hati ya mashtaka, Malima anadaiwa kuwa Mei 15, mwaka huu katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia ofisa wa polisi mwenye namba  H.7818 PC Abdul kufanya kazi yake halali wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari lake alimshambulia na kumsababishia maumivu

No comments:

Post a Comment