Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa
kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu ambapo inaonyesha
kutakuwa na mvua za wastani katika maeneo mengi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Agnes Kijazi
amesema mvua zinatarajia kuwa za wastani katika maeneo ya mikoa ya
Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Shinyanga, Dar es salam, Tanga, Pwani,
Kilimajaro, Arusha, na Manyara ambapo katika maeneo ya Kazikazini mwa
mkoa wa Morogoro na Visiwa vya Unguja, Pemba utabiri wake utatolewa
mwanzoni mwa mwezi Oktoba .
Aidha Kijazi amesema, katika Ukanda wa Pwani ya Kazikazini (Dar es
salam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Uguja na Pemba) na maeneo ya Kaskazini
mwa Mkoa wa Morogoro, msimu huu wa mvua unatarajia kuanza wiki ya
kwanza hadi ya pili ya mwanzoni mwa mwezi Oktoba na kuisha wiki ya nne
ya mwezi Disemba ambapo katika Kanda ya Nyanda za Juu Kaskazini
Mashariki (Kilimajaro, Arusha na Manyara) mvua hizo zitaanza wiki 3 ya
mwezi Novemba na kuisha wiki ya 4 ya mwezi Decemba mwaka huu.
Kijazi ametoa ushauri kwa sekta mbalimbali ikiwepo sekta ya kilimo
ili kuandaa pembejeo mapema kwa ajili ya wakulima na kwa upande wa
wakulima wameshauriwa kuandaa mashamba mapema ili kuendana na msimu wa
mvua.
No comments:
Post a Comment