Baadhi
ya Maafisa Waandimizi wa Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa
bidhaa za Kilimo kutoka wakulima kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia
taarifa mbalimbali zilizotolewa na Wenyeviti wa Mkutano huo uliojadili
changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na uwekezaji katika
Mataifa hayo.
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. Pindi Chana akitoa taarifa ya
majadiliano ya mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Tanzania
na Kenya uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na
uwekezaji katika Mataifa. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini
Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara
ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya
Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Baishara na
Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Watendaji Wakuu wa
Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika
Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es
Salaam. Wengine katika Picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya
Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya
Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano wa Kenya, Dkt. Chris
Kiptoo akizungumza na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wafanyabiashara na
Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika Mataifa hayo. Mkutano huo
ulifanyika jana Septemba 8 Jijini Dar es Salaam. Wengine katika Picha ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Tanzania, Prof. Adolf Mkenda na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Kenya Dkt. Chris Kiptoo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kenya, Dkt.
Chris Kiptoo na Mwenjeji wake Prof. Adolf Mkenda wakionyesha Sera ya
Taifa ya Biashara ya Kenya wakati mkutano baina ya Watendaji Wakuu wa
Serikali, Wafanyabiashara na Wazalishaji wa bidhaa za kilimo katika
Mataifa hayo uliojadili changamoto na utatuzi wa vikwazo vya biashara na
uwekezaji katika Mataifa hayo. Mkutano huo ulifanyika jana Septemba 8
Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO)
HABARI KAMILI
SERIKALI
za Tanzania na Kenya zimekubaliana kwa pamoja kumaliza vikwazo vya
kibiashara katika usafirishaji na uingizaji wa bidhaa katika mipaka
baina ya nchi hizo mbili hatua inayokusudia kuimarisha ushirikiano wa
biashara na uwekezaji katika Mataifa hayo.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara,
Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda mara
baaada ya kumalizika kwa mkutano wa pamoja yao ulioshirikisha Viongozi
Waandamizi wa Serikali hizo, Wafanyabiashara na Wakulima kutoka Mataifa
hayo.
Anasema
katika mkutano huo Serikali ya Tanzania iliwasilisha mapendekezo 15 kwa
Serikali ya Kenya yanayopaswa kupatiwa ufumbuzi, ambapo kwa upande wa
Kenya waliwasilisha mapendekezo 16 ambapo kwa kiasi kikubwa hoja hizo
zimekubaliwa na kupatiwa majibu yake katika mkutano huo.
Prof.
Mkenda alisema kupatikana kwa mwafaka wa majadiliano hayo ni maelekezo
ya Viongozi Wakuu wa Mataifa hayo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa
Tanzania na Uhurru Kenyatta wa Kenya kwa kuwa Viongozi hao wametaka
suala hilo lipatiwe mwafaka wa haraka ili kuweza kuendeleza ushirikiano
na uhusiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo.
Kwa
mujibu wa Prof. Mkenda alisema mkutano huo uliofanyika kwa muda wa siku
tatu ulilenga kumaliza changamoto za biashara zinazojitokeza kwa
Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, ambapo Timu za Wataalam wa
Serikali hizo ambapo hoja hizo zimeweza kujadiliwa na kupatiwa ufumbuzi
wa pamoja, hatua inayolenga kufungua upya milango ya ushiriakiano baina
ya Wafanyabiashara na Wakulima wa Tanzania na Kenya.
“Katika
majadiliano yetu tumekubaliana kuwa sasa bidhaa ya gesi ya kupikia na
ungano wa ngano ambazo zilizuliwa kuingia Kenya sasa zitaruhusiwa
kuingia nchini humo, na sisi kwa upande wetu Tanzania tumeruhusu maziwa
na sigara kutoka Kenya zianze kuingia nchini” alisema Prof. Mkenda.
Akifafanua
zaidi Mkenda anasema Mkutano huo pia uliwashirikisha Wafanyabiashara na
Kampuni za uzalishaji wa bidhaa za ngano ikiwemo kampuni ya Azam
Bakhressa ambayo huzalisha na kusambaza ngano hapa nchini pamoja na nchi
jirani ikiwemo Kenya pamoja na wakulima wa zao hilo kutoka mikoa ya
Sumbawanga, Iringa na Manyara.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Ushirikiano
ya Kenya, Dkt. Chris Kiptoo alisema Serikali ya Kenya itayachulia kwa
uzito unaostahili mwafaka wa majadiliano hayo, kwa kuzingatia kuwa
Serikali ya Tanzania na Kenya zina uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu
katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Alisema
kuwa Serikali ya Kenya imewekeza jumla Dola Bilioni 1.5 katika sekta ya
viwanda, ambapo hadi sasa vimeweza kuajiri jumla ya watu 50,000 na pia
msingi wa biashara ya Kenya katika Tanzania imeweza kuongeza kutoka Tsh.
Bilioni 17 mwaka 2004 hadi kufikia Dola Bilioni 34 mwaka 2015.
Dkt.
Kiptoo anasema mara baada ya mkutano huo, Viongozi wa Serikali hizo
pamoja na Wafanyabiashara kutoka upande za Tanzania na Kenya wanatarajia
kukutana kwa mara ya mwisho Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya
kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya uingizaji na usafirishaji wa
bidhaa.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kiptoo anasema katika majadiliano hayo Idara muhimu
zinazohusika na masuala ya biashara na uwekezaji kutoka Serikali za
Tanzania na Kenya zilishiriki katika mkutano huo, ikiwemo Maafisa wa
Idara za forodha, kodi na ushuru.
Tarehe
3 Agosti mwaka huu, Viongozi Waandamizi wa Serikali za Tanzania na
Kenya walikutana katika Mpaka wa Namanga kwa ajili ya kikao cha
majadiliano ya pamoja kilicholenga kumaliza mzozo wa kuzuiwa kwa
Wafanyabiashara ya Ngano nchini kuingiza bidhaa hiyo nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment