Ripoti ya Makinikia ya Almasi na Tanzanite: Mruma, Maswi na Muhongo washutumiwa - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 6 September 2017

Ripoti ya Makinikia ya Almasi na Tanzanite: Mruma, Maswi na Muhongo washutumiwa


Aliyewasirisha Ripoti hiyo ni mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu na anaongelea kamati iliyoyabaini ikiwemo kutowajika kwa mamlaka zinazohusika na almasi na Tanzanite ikiwemo NEMC na wizara ya nishati na madini.
Kamati ilibaini kutolipwa kwa income tax ikiwa kinyume na kifungu cha kodi kinacholazimisha kampuni za madini kulipa kodi. Kampuni ya Williamson haijalipa income tax kutoka 2007 mpaka 2017 kwa kisingizio cha kupata hasara.

Mapato stahiki nchi inatakiwa kupata ni kodi kwani mrahaba ni kiasi kidogo ambacho huwa ni fidia. Kuna mkanganyiko wa takwimu kwenye mauzo ya almasi. Kuna takwimu zinazokinzana ambapo nishati na madini na wakala wa madini(TIMA) umebaini kutofautiana kwa takwimu kutoka taasisi hizo mbili za serikali.


  • Kamati imebaini kwenye vyumba ambavyo Almasi huwa inahifadhiwa, kuna milango ya dharura ambayo hutumiwa vibaya.
  • Serikali inapata hasara kubwa kutokana na usafishaji wa Almasi nje ya nchi ambao hudaiwa kuwa inapungua thamani.
  • Kamati imeona kuna haja usafishaji wa mwisho wa madini ya Almasi ufanyike hapa nchini kwani haihitaji uwekezaji mkubwa.
  • Kutokana na kukosa mapato stahiki, kuna haja ya Serikali kupitia misamaha yote ya kodi ya madini ya Almasi hapa nchini.

Thamani ya Madini ya Almasi yanayouzwa nje ya nchi ni kubwa zaidi ukilinganisha na kodi inayolipwa hapa nchini.

  • Kwa maoni ya kamati kwa uamuzi wa serikali kutoinunua Petra kwa dola milioni 10 umesababisha hasara kwa sababu kwa sababu mgodi umezalisha almasi zenye thamani ya dola milioni 343. De Beers waliuza hisa bila kufata utaratibu, kamati ikiongozwa na waziri wa wakati huo, Ngonyani walitoa ushauri usinunuliwe.
  • Viongozi wa serikali waliopendekeza mgodi usinunuliwe ndio waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bodi.
  • Kamati ilipowahoji wajumbe wa bodi, Professa Jairo na Prof Mruma chini ya kiapo, Prof Mruma aliiambia kamati alishindwa kufuatilia madeni(Akiwa mwenyekiti wa audit commitee ya mgodi) kwa sababu hakuwa na muda wa kusoma na aliawaamini waliompelekea taarifa hizo baada ya kamati kumuhoji madeni yaliyobambikwa kwa serikali yamekuwa ni mengi mno.

  • Kamati ilimuhoji mheshimiwa Maswi ambae alikuwa katibu mkuu na ni mmoja alietia saini mkataba ambao kamati inaona una utata, alijibu hata yeye aliona kilichofanyika ni upuuzi mtupu na alienda mara moja Tanzanite one na alichukia na kutorudi tena ilhali akiwa ndie msimamizi wa wizara.

  • Kamati imebaini kuna zawadi ilitolewa kwa kiongozi mmoja mkubwa, zawadi hio ya almasi kwa sasa inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 200.
  • Makinikia yaliyobakiwa yanakadiriwa kuwa na thamani inayokadiriwa kuwa trilioni 2.3. Kamati inahoji mbona taarifa haikutolewa na yalichimbwa na marehemu Wilamson miaka ya 50? Wataalam wahakikishe gharama za makinikia hayo hazijumuishwi kwenye gharama za mgodi.

Inasikitisha kuona watumishi wa serikali hawajui kinachoendelea kwenye makampuni ambayo walipaswa kuyasimamia.

Zungu amempongeza Rais Magufuli kwa kuliamsha dude na wao wanaendelea nalo

No comments:

Post a Comment