Rais Magufuli Agoma Kusaini Waliohukumiwa Kunyongwa - TANZA MEDIA ONLINE

Monday 11 September 2017

Rais Magufuli Agoma Kusaini Waliohukumiwa Kunyongwa

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma
kutompelekea orodha ya wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ili aidhinishe
kunyongwa kwao kwani anafahamu ugumu ulivyo wa kufanya hivyo.


Rais Magufuli ameyasema hayo katika
halfa ya kumuapisha aliyekuwa Kaimu Jaji Mkuu kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania
baada ya jana kuteuliwa rasmi kushika wadhifa huo.

“Ninafahamu
baadhi ya wafungwa hawa wapo wengi wanaosubiri kunyongwa hadi kufa, na
marais waliopita walikwepa jukumu la kusaini sheria hii, na mimi
nakuomba Jaji Mkuu usiniletee kwa sababu nafahamu ugumu wake,”
alisema Rais Magufuli.


Tamko hilo la Rais Magufuli limeungwa
mkono na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambapo wamesema
kwamba sheria ya kifo inakiuka haki ya kuishi na inatweza utu wa
binadamu.

Kwa upande mwingine
Rais Magufuli amewapongeza majaji wote waliopo kazini na wastaafu na
kusema kwamba wanafanya/walifanya kazi kubwa ya kuwatumikia wananchi.


Kwa upande wake Jaji Mkuu, miongoni mwa
mambo mengi aliyoyazungumza ni pamoja na kutolea ufafanuzi taarifa
ambazo zimekuwa zikisambazwa na watu kuwa kuna muingiliano katika
mihimili ya serikali.


Akitolea ufafanuzi hilo alisema si
kweli kwamba kuna muingiliano unaodaiwa, bali kuna wakati muhimili hiyo
lazima ikae pamoja kuwatumikia wananchi lakini kila mmoja una majukumu
yake ya kutekeleza.

KWA HABARI ZAIDI TIZAMA VIDEO HII HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment