KIONGOZI
wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari
kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo. Amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.
Odinga pia anataka mabadiliko kufanyiwa
Tume ya Uchaguzi nchini humo, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa
wa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa nzuri ambayo ilisababisha
kufutia matokeo.
Jana Jumatatu, Tume ya Taifa ya
uchaguzi nchini Kenya ilitangaza kwamba uchaguzi mpya wa urais nchini
humo utafanyika tarehe 17 Oktoba.Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula
Chebukati alisema uchaguzi huo utashirikisha wagombea wawili pekee wa
urais, Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga.
“Hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea
wa urais katika uchaguzi huo upya. Waliopinga matokeo ya uchaguzi
kortini, Bw Raila Odinga na mgombea mwenza wake Stephen Kalonzo Musyoka
na mshtakiwa wa tatu Rais Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William
Samoei Ruto, watakuwa ndio wagombea pekee,” taarifa ya bw Chebukati
ilisema.
Katika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti, Mahakama ya Juu iliiwekea lawama Tume ya Uchaguzi
No comments:
Post a Comment