Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Mh. Zitto
Kabwe amefunguka na kusema kuwa Spika wa Bunge Job Ndugai ameibuka
sakata lake yeye ili kutaka kufunika nguvu ya wananchi kuhoji juu ya
kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu.
Zitto Kabwe amesema hayo leo mara tu baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai leo bungeni kusema anauwezo wa kumzuia Mbunge huyo asizungumze bungeni hadi mwisho wa bunge hilo kwani Zitto hawezi kupambana naye.
"Nimegundua Spika Ndugai ameibua mashtaka yangu ili kufunika ufuatiliaji wa wananchi kuhusu Tundu Lissu kupigwa risasi. Nimeamua sitawapa hilo" aliandika Zitto Kabwe kupitia mtandao wake wa Twitter
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai jana aliagiza Mbunge Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea kufika kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kuhojiwa kutokana na kauli walizotoa hivi karibuni, jambo ambalo Zitto Kabwe anadai limeibuliwa kwa lengo la kupunguza nguvu ya wananchi kutohoji sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi

No comments:
Post a Comment