UFAFANUZI: NECTA kuhusu shule zifanyazo udanganyifu Mitihani ya Taifa
Baraza la Mitihani Tanzania ‘Necta’
limeeleza kuwa shule zote zinazofungiwa kuwa vituo vya mitihani kutokana
na sababu za ukiukwaji wa kanuni za baraza hilo wakati wa mitihani ya
kitaifa haimaanishi shule hizo zinafungiwa kabisa kufundisha bali
zinafutiwa kibali cha kuwa vituo vha kufanyia mitihani.
Katibu Mtendaji wa NECTA Dr. Charles Msonde amesema shule hizo
zinaedelea na shughuli zake za kufundisha wanafunzi kama kawaida lakini
unapofika wakati wa mitihani Baraza na Mamlaka husika huwapeleka
watahiniwa hao kwenye kituo kingine ili kufanya mitihani yao.
”Tunapofungia kituo
pale tunapoona kuwa kituo hicho sio salama tena mitihani kufanyika hapo
kwani inawezekana kituo hicho kikatumika kusambaza mitihani nchi nzima
na hivyo ni hatari kwa usalama wa taifa kwa ujumla.” – Dr. Msonde.
aidha pia katibu mkuu Msonde ameeleza kuwa darasa la saba wote nchini watanza mitihani yao ya mwisho kesho tarehe 06/09/2017 hadi 07/09/2017
No comments:
Post a Comment