SERIKALI ya Marekani inayoongozwa na
Rais Trump kupitia ubalozi wake ulioko hapa nchini, imeeleza
kusikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu.
“Marekani imesikitishwa sana kuhusu
kupigwa risasi kwa Tundu Lissu, Mbunge na Rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika. Tunalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu.
Tunaungana na Watanzania kutoa matumaini yetu ya dhati ili apone haraka.
———————————
The United States is deeply
saddened by the shooting of Tundu Lissu, Member of Parliament and
President of the Tanganyika Law Society. We condemn this senseless act
of violence and join Tanzanians in expressing our sincere hopes for his
full and speedy recovery.” Imesema taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Ubalozi huo umesema unaungana na
Watanzania katika kumtakia kheri Lissu ambaye pia ni Rais wa C
Lissu jana Alhamisi saa sita usiku alisafirishwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya.
Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma baada ya kushambuliwa. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema leo Ijumaa asubuhi kuwa, Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.
Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.
Aidha, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji amesema kuwa amepokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kuwa Tundu Lissu amezinduka
leo asubuhi akiwa katika Hospitali ya Aga-Khan jijini Nairobi nchini
Kenya, kwa sasa ameshazinduka anajitambua na anaendelea vizuri.
Pia ametaja AKAUNTI YA KUCHANGIA MATIBABU YA MHE. TUNDU A.
LISSU NI CRDB BENKI/ TAWI LA MBEZI JINA LA AKAUNTI NI : CHADEMA M4C
01J1080100600
No comments:
Post a Comment