“Kama jambo haulijui na haujalishiriki bora……”-Ridhiwani Kikwete - TANZA MEDIA ONLINE

Monday 11 September 2017

“Kama jambo haulijui na haujalishiriki bora……”-Ridhiwani Kikwete

Image result for ridhiwani kikweteMchana wa September 7 2017 taarifa za Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi akiwa ndani ya gari lake maeneo ya nyumbani kwake Area D Dodoma na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa. 
 
Taarifa zilizokuwa zinaripotiwa katika mitandao ya kijamii ni kuhusiana na madai ya kuwa, Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana waliyokuwa wakimfuatilia wakiwa ndani ya Nissan nyeupe, tukio ambalo bado polisi wanaendelea na upelelezi wa kubaini ukweli.

Baada ya mijadala kuwa mingi mtandaoni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe unaolenga kuhamasisha watu kuwa watukivu na kusubiri vyombo husika kuleta majibu.

“Kama jambo haulijui, haujalishiriki bora Unyamaze. Kutunga Uongo au kuandika sana ili kuonekana unajua sana kufikiri dhidi ya uhalisia hakutasaidia upelelezi wala Haki kuonekana ikitokea. Tuwe watulivu kipindi hiki ili Haki itokee” Ridhiwani Kikwete

No comments:

Post a Comment