WABUNGE wa Kambi ya Upinzani Bungeni
wamesusia kuapishwa kwa wabunge saba Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi
(CUF) katika mkutano wa nane Bunge la 11 kwa madai hawakufurahishwa na
maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama hicho.
Mkutano wa nane wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania umeanza leo Mjini Dodoma
na moja ya mambo yaliyopo kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa
wabunge 7 wapya kati ya 8 wa Viti Maalumu ambao waliteuliwa kuziba
nafasi za wabunge wa Viti Maalumu waliofutwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba baada ya kupoteza sifa ya kuwa wabunge.
Wabunge ambao wamekula kiapo cha
uaminifu siku ya leo Septemba 5 ni pamoja na Alfredina Kaigi, Kiza
Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na
Zainab Amir.
Aidha, CUF kimewaapisha wabunge saba
badala ya nane kama inavyotakiwa kutokana na mbunge mmoja mteule Hindu
Mwenda kufariki siku ya Ijumaa Septemba Mosi katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili.
Kwa upande mwingine, wabunge wa upinzani waliingia bungeni baada ya wabunge hao kumaliza kuapishwa na Spika Job Ndugai.
No comments:
Post a Comment