Rais Uhuru Kenyatta, akihutubia baada ya kutangazwa mshindi wa urais
wa Kenya, amewashukuru wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali
yake.
“Nawaahidi tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Wakenya. Kadhalika, naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” amesema.
“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”
Kwa upinzani amesema: “Sisi si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila
shindano, kutakuwa na washindi na wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa
Wakenya. Nawapa moyo wa ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya
wanataka sisi tufaulu.
“Sana kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote
waliochaguliwa kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana,
tutakua pamoja na kuendeleza nchi pamoja.
“Kwa Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya
itaendelea kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani
yako bado ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya
fujo, sisi wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”
VIDEO: Rais Uhuru Kenyata akihutubia baada ya kutangazwa mshindi
No comments:
Post a Comment