SERIKALI YAANZA KUSAMBAZA MRADI WA GAS MAJUMBANI - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday 22 August 2017

SERIKALI YAANZA KUSAMBAZA MRADI WA GAS MAJUMBANI

Kamati ya Bunge ya Bajeti ilifanya ziara katika Kituo cha kupokea gesi Kinyerezi I na II ikiwa ni mchakato wa kuhakiki matumizi ya bajeti zilizotengwa na Serikali katika mradi huo.
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema tayari utaratibu umeanza kufanyiwa majaribio kwa gesi hiyo kuanza kusambazwa majumbani kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni pamoja na kupikia.


”kuifanya hii gesi itumike majumbani. Tumeanza utaratibu wa upembuzi yakinifu unakamilika. Tumashaunganisha wananchi Sabini wanaotumia gas majumbani. Umeanza kwa mradi wa mfano Mikocheni na Kijitonyama".

“Tukitoka hapo itakuwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam, Pwani kisha tunakwenda Mtwara pamoja na Lindi.” – Naibu Waziri Kaleman.

No comments:

Post a Comment