RONALDO AFUNGIWA MECHI TANO - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday 15 August 2017

RONALDO AFUNGIWA MECHI TANO

Ronaldo akipigwa kadi nyekundu.
Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefungiwa kutocheza mechi tano kutokana na kumsukuma mwamuzi katika mchezo dhidi ya Barcelona, jana usiku.
Shirikisho la Soka la Hispania limemfungia Ronaldo michezo mitano huku moja kati ya mchezo huo ni fainali ya pili ya Super Cup dhidi ya Barcelona.
Ronaldo Akimsukuma refa.

Michezo mingine utakuwa dhidi ya Deportivo, dhidi ya Valencia dhidi ya Levante na wa mwisho utakuwa dhidi ya timu ya Real Sociedad na atarudo mwezi wa 9 kwenye mchezo dhidi ya Real Betis.
Ronaldo Akisikitika baada ya kupewa red card.

Mechi 5 ambazo Ronaldo atazikosa;
Barcelona- 16 Agosti
Deportivo- 20 Agosti
Valencia- 27 Agosti
Levante- 9 Septemba
Real Sociedad- 17 Septemba

No comments:

Post a Comment