Mkazi wa kijiji
cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi
Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari
polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda wa Jeshi
la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo
limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha
Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.
Amefafanua kuwa
Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu
kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358
na risasi zake tano.
Amesema bunduki
hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa
kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa
sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.
ACP Magiligimba
amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji
cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa
tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.
“Kesho yake
mtuhumiwa alihojiwa na kukiri kujihusisha na matukio ya ujambazi wa
kutumia silaha katika mikoa mbalimbali. Pia aliahidi kuwapeleka askari
kuwaonyesha mahali alikoificha silaha anayoitumia kwenye matukio hayo ya
ujambazi,” amesema ACP Magiligimba.
Kamanda huyo
amesema Agosti 25 mwaka huu saa sita mchana, askari polisi wakiwa na
mtuhumiwa, walikwenda katika pori la kijiji cha Mgori mahali alipokuwa
ameficha bunduki hiyo aina ya rifle.
“Mara tu
baada ya kuwaonyesha askari hao silaha hiyo na wakati askari wanaendelea
kufanya upekuzi katika eneo hilo, mtuhumiwa alijaribu kutoroka askari
kwa kukimbia” amesema na kuongeza.
“Askari mmoja
alifyatua risasi tatu hewani akimtaka asimame, lakini hakutii. Ndipo
alipompiga risasi moja iliyompata sehemu ya kiunoni”.
Amesema jereha
hilo la risasi lilisababisha mtuhumiwa Hamisi avuje damu nyingi, na
hivyo kufariki dunia wakati akikimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.
“Jeshi la
Polisi Mkoa wa Singida linaendelea kutoa wito kwa wananchi waote kutoa
taarifa zitakazosaidia kubaini wahalifu katika maeneo yao ili hatua
ziweze kuchukuliwa kudhibiti vitendo vya kihalifu,” amesema kamanda huyo.
No comments:
Post a Comment