Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 imepokea taarifa
ya Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyoonesha kuwa
sampuli ya mkojo wa Agnes Gerald maarufu kama Masogange una chembechembe
za dawa za kulevya.
Taarifa hiyo imepokelewa baada Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri
kutoa uamuzi wake ambapo amesema Mahakama imepokea taarifa hiyo na
pingamizi la utetezi limetupiliwa mbali.
Pingamizi la upande wa utetezi ni kwamba fomu zilizopelekwa kwa Mkemia Mkuu hazikufuata sheria.
Hakimu Mashauri amesema Mkemia huyo Elia Mulima ambaye ni Shahidi wa
kwanza ana haki ya kuandaa ripoti, kupima sampuli na kutoa ripoti
Mahakamani.
Kuhusu hoja ya kuwasilishwa maombi ya kupimwa mkojo Masogange, Hakimu
amesema ni wazi Polisi walipeleka maombi kwa Mkemia na mshtakiwa
alienda akiwa chini ya askari wawili, ambapo walipatiwa kontena kwa
ajili ya kuweka sampuli ya mkojo wa Masogange.
No comments:
Post a Comment