Mfanyabishara Yusuf Manji amefikishwa tena mahakamani leo August 10,
2017 dhidi ya kesi utumizi wa madawa ya kulevya. ambapo upande wa Serikali umeileza Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu itafika na mashahidi wasiozidi 10 katika kesi ya kutumia na
kujihusisha na dawa za kulevya inayomkabili mfanyabiashara huyo.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis mbele ya
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya kumsomea Manji maelezo ya awali
(Ph) ambapo katika maelezo hayo, Vitalis amedai mshtakiwa ni mkazi wa
Sea view DSM, pia ni mfanyabiashara anayetuhumiwa kujihusisha na kutumia
dawa za kulevya.
Amedai kuwa alikamatwa February 2, 2017 kisha akapelekwa kituo cha
Polisi ambapo alichukuliwa hadi nyumbani kwake na kupekuliwa na baada ya
kupekuliwa alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kuchukuliwa haja
ndogo (Mkojo) ambao ulipimwa na kukutwa na dawa za kulevya aina ya
Benzodiazepine.
Baada ya kusomewa maelezo hayo, Manji alikubali wasifu wake kwamba ni
mfanyabiashara, makazi na jina lake licha ya kudai limekosewa ila
usahihi ni Yusufali Manji huku akikana maelezo mengine.
Aidha, wakili Vitalis ameieleza Mahakama kwamba wanaomba kupangiwa
tarehe kwa ajili ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa, pia wanatarajia kuwa
na mashahidi wasiozidi 10 hivyo Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi
August 22, 23, na 24, 2017 kwa ajili ya kusililizwa mfululizo.
No comments:
Post a Comment