KESI inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutuhumiwa na
matumizi ya dawa za kulevya leo Ijumaa, Agosti 22, 2017 imeanza kutolewa
ushahidi wa vipimo vilivyochunguzwa kwa mkemia mkuu wa serikali na
majibu yake huku wakili wake akipinga kielelzo hicho cha mkojo hakikuwa
halali.
Ushahidi huo umeanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha
kwa nyakati tofauti shahidi wa kwanza alikuwa Ofisa Mkuu wa Makosa ya
Jinai na Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es Salaam, Ramadhan
Kindai na Askari Polisi Kitengo cha Upelelezi cha Makosa ya Jinai,
Christopher.
Wakifafanua mahakamani hapo wameeleza
hatua zote walizozifuata tangu Manji aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi,
Februari 9 mwaka huu na kupelekwa kwa mkemia kwa ajili ya kuchukuliwa
vipimo vya mkojo na hatimaye kugundulika anatumia madawa ya kulevya.
Kwa upande wa utetezi, Wakili wa Manji,
Hoodson Ndusiepo aliukataa ushahidi wa barua iliyoandikwa ya Manji
kupelekwa kwa Mkemia Mkuu ili kuchukuliwa vipimo vya mkojo kwa madai
kuwa barua hiyo ilitakiwa kuwa na sahihi ya mteja wake kuridhia
akachukuliwe vipimo hivyo.
Pia wakili huyo alimhoji shahidi wa kwanza juu ya
hati ya mashtaka iliyofunguliwa dhidi ya Manji inayoonesha mteja wake
anatuhumiwa kwa matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine na kwa nini inatofautiana na vipimo vya mkemia vinavyoonyesha aina ya madawa yaliyogundulika wakati wa vipimo kuwa aina ya Benzodiazepine.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkeha ameiahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano, Agosti 23.
TIZAMA VIDEO YA MAHAKAMANI LEO
No comments:
Post a Comment