MSANII mkongwe wa filamu nchini, Jacob Steven ‘JB’ ametangaza
kujiengua katika uigizaji na sasa ameanzisha Taasisi ya Barazani
Entertainment ili kulinda heshima yake.
Katika mahojiano maalum katikati ya wiki hii, JB ambaye anachukuliwa
kama mmoja wa waigizaji mahiri kuwahi kutokea, hajaondoka moja kwa moja
katika filamu bali amebadili nafasi na sasa atakuwa msambazaji.
“Nimeshakuwa muigizaji na mtengenezaji na nimekuwa nikipeleka filamu
zangu na wenzangu mahali palepale siku zote, halafu tunapanga foleni
kusubiri kulipwa. Sasa unapofikia hatua kama hii, lazima utazame nje ya
boksi.
“Naachana na filamu na kuwaachia vijana ili nitunze heshima yangu, maana nikiendelea, iko siku watanivunjia heshima ambayo nimeijenga kwa miaka mingi,” anasema JB.
“Naachana na filamu na kuwaachia vijana ili nitunze heshima yangu, maana nikiendelea, iko siku watanivunjia heshima ambayo nimeijenga kwa miaka mingi,” anasema JB.
“Wasanii tumejichangisha na kuunda taasisi iitwayo Barazani
Entertainment, hii itahusika na usambazaji filamu kwa njia za kisasa
zaidi. Ni mtandao unaohitaji muda, lakini nikuhakikishie kwamba haya ni
mapinduzi makubwa katika filamu.
“Barazani Entertainments itaajiri kijana mmoja, ambaye sisi tutamuita
venda, kwa kila nyumba 500 nchi nzima. Katika eneo hili, tunategemea
kuwa ajili zaidi ya vijana 9000. Kazi yao itakuwa ni kusambaza filamu
kwa haraka popote itakapohitajika.
“Kwa mfano, kama mtu anataka kununua filamu na yupo Chato, ndani ya
saa moja filamu hiyo itakuwa barazani kwake, kwa sababu nyumba ya mteja
huyo itakuwa miongoni mwa nyumba 500 za venda wetu. Ndiyo maana tunaitwa
Barazani kwa sababu itakufikia hapo hapo ulipo.
“Kwa wasanii, kwanza hata kama wana wazo tu la filamu na hawana
fedha, wakija kwetu na tukakubaliana na wazo lake, atatengenezewa filamu
na kuiingiza sokoni halafu tutakatana zile gharama baada ya mauzo,”
anasema JB.
Kuhusu kudorora kwa soko la filamu nchini, JB anasema: “Tatizo tasnia iliingiliwa, kila mtu anadhani anaweza kuwa msanii, mwongozaji au mtengeneza skripti, tulichodhamiria kukifanya ni kwamba tutasambaza filamu zenye ubora tu na hii tutausimamia wenyewe, tunataka tasnia irudi katika mstari ulionyooka.”
No comments:
Post a Comment