Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa
ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi
lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar
Kongamano
la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora
Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha
washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria
zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa
ni 150.
Diaspora
wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya
kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira
yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu
Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania
waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017
katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya
Magharibi A.
Mhe
Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na
serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa
kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa
uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.
Alisema
kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna
changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa
uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini
changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.
Changamoto
zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe
Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo
katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Alisema
serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze
kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia
fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa
Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema
kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya
maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika
uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao
kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.
Alisema
kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni
mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi,
fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega
uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na
uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.
Aidha,
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za
kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali
kujiendesha.
Mhe
Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi
wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na
wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la
Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa
minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna
ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano
hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka
2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini
Zanzibar.
Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana,
kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao
kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.
Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”
Katika
hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja
namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi
sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na
ushirikiano bora kati yao na serikali.
Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.
No comments:
Post a Comment