BAADA YA SAKHO KUFELI VIPIMO VYA KUTUMIA MADAWA, HII NDIYO ADHABU INAYOMKABILI - TANZA MEDIA ONLINE

Sunday, 24 April 2016

BAADA YA SAKHO KUFELI VIPIMO VYA KUTUMIA MADAWA, HII NDIYO ADHABU INAYOMKABILI

Sakho
Ile issue ya kesi inayomkabili beki wa Liverpool Mamadou Sakho ya kufeli kwenye vipimo vya kutumia madawa ya kusisimua misuli imekuwa gumzo kubwa kwenye magazeti ya England siku ya Jumapili April 24.

Sakho hakuwepo kwenye kikosi cha Liverpool kilicholazimishwa sare ya kufungana bao 2-2 na Newcastle kwenye mchezo wa ligi siku ya Jumamosi baada ya beki huyo wa kifaransa kushindwa kufuzu kwenye vipimo alivyofanyiwa kwenye mchezo wa Europa League v Manchester United.
UEFA imemtaka Sakho kukabidhi sample B siku ya Jumanne kwa ajili ya vipimo vya uhakiki la sivyo akubaliane na kesi inayomkabili.
Mchezaji huyo wa Liverpool huenda akakabiliwa na adhabu nzito kutoka UEFA. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Sakho huenda akaikosa michuano ya Euro 2016 itakayofanyika kwenye ardhi ya Ufaransa wakati wa majira ya joto mwaka huu na huenda asikitumikie kikosi cha Jurgen Klopp hadi mwezi October kutokana na kufeli vipimo hivyo.
Gazeti la The Sunday Times pia limethibitisha kwamba, Sakho huenda akakumbana na adhabu ya kufungiwa kucheza soka kwa miezi 6 endapo atakutwa na hatia ya kutumia madawa yaliyozuiwa kwenye michezo, huku gazeti hilo likitoa taarifa za ndani kuhusiana na kesi hiyo.

No comments:

Post a Comment