WATANZANIA WAPATA SHAVU TUZO ZA FILAMU ZA AFRICAN MAGIC PEOPLES CHOICE NIGERIA - TANZA MEDIA ONLINE

Friday 4 March 2016

WATANZANIA WAPATA SHAVU TUZO ZA FILAMU ZA AFRICAN MAGIC PEOPLES CHOICE NIGERIA


LULU

Watanzania watakuwa sehemu ya wale watakaoshiriki katika tuzo maarufu za African Magic Peoples Choice Awards.

Tuzo hizo zinatarajia kufanyika kesho jijini Lagos nchini Nigeria na Watanzania wasanii wa filamu wamepata nafasi.

Msanii mkongwe wa filamu nchini Richie Richie, yeye amefanikiwa kuingia kwenye vipengele viwili vya Best East African na Best Swahili kupitia filamu ya Kitendawili.


HONEYMOON

Mwanadada Honeymoon Mohammed ambaye ni muongozaji ameingia katika kipengele cha East African kupitia filamu yake ya DADDY’S WEDDING.


Wengine ni Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye anaingia katika kipengele cha East African pia, Ameir Shivji katika kipingelea cha Best Swahili kupitia filamu ya Samaki Mchangani huku Mtanzania mwingine akiingia kwenye kipengele cha East African kupitia filamu ya Mpanngo Mbaya.

No comments:

Post a Comment