MUENDELEZO WA CHOKOCHOKO ZA NAY WA MITEGO V/S BONGO MOVIE - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday 4 February 2016

MUENDELEZO WA CHOKOCHOKO ZA NAY WA MITEGO V/S BONGO MOVIE



Niva na nay wa mitego
Msanii wa Bongo Movie Tanzania Niva ‘Super Mario’ amesema hana mpango wa kumshitaki msanii wa Bongo Fleva Ney wa Mitego baada ya kumkashifu kuwa ‘hana hata pa kulala,analala kwenye gari‘.
Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo wa bongo Fleva kuwarushia maneno wasanii wa bongo movie ikiwemo Niva kuwa pesa zote wanazozipata zinaishia kwenye mambo yasiyo na tija.Tetesi zimeenea kuwa baadhi ya wasanii hao wamepanga kumfungulia mashitaka Ney wa Mitego kwa kile walichokiita kuwadharirisha.
“Ney ni mdogo wangu siwezi kumfanya chochote,nimesoma nae,ni mwanangu mwache aseme tu anavyojisikia..wapo watu na wanasheria walionifata kunishauri nimchukulie hatua za kisheria ila sina mpango huo” alifunguka Niva ambaye alikanusha kashfa hiyo kwa kusema yeye anamiliki nyumba na anayamudu maisha yake.

No comments:

Post a Comment