Siku chache baada ya Simba kupokea kichapo cha bao 2-0 kutoka kwa
Yanga kwenye mchezo wa VPL, kocha wa timu ya Simba Jackson Mayanja
amefunguka na kusema kilichosababisha timu yake kushindwa kuibuka na
ushindi kwenye mchezo dhidi ya wapinzani wao kwenye soka la Bongo.
“Vitu tulivyovifanyia mazoezi wakati wa maandalizi na plan ya mechi
dhidi ya Yanga, wachezaji wangu walifanya tofauti. Lakini wangecheza
kama vile tulivyokuwa tumeelekezana wakati wa mazoezi nafikiri
tungefanya vizuri”, anafafanua kocha huyo ambaye amepoteza mchezo wa
kwanza kati ya saba tangu atue Simba.
“Watu wanaosema kwamba nilikosea kumpanga Kiiza mbele ya beki mrefu
kama Bossou inawezekana hawajui kabisa mpira, ingekuwa hivyo basi akina
Maradona na Messi wasingecheza soka. Kiiza sio mara ya kwanza kucheza
mbele ya mabeki warefu ameshacheza mechi nyingi za kimataifa mbele ya
wanigeria na wasenegal na akawafunga. Lakini wakumbukuke kuwa Kiiza
ndiyo anaongoza kwa kufunga kwenye ligi hadi sasa”.
“Lakini kwasababu tumepoteza mchezo kila mtu anaongea la kwake lakini
mimi sitaki kusema mambo mengi ya kiufundi zaidi ila wachezaji
hawakucheza kama tulivyofanya mazoezi kabla ya mchezo dhidi ya Yanga”.
“Ligi bado, mechi ya Yanga siyo mechi pekee ya ligi. Sasahivi
tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo za ligi pamoja na FA tuone
tutaifikisha wapi Simba.
“Nawashukuru mashabiki wote wa Simba waliojitokeza kuishangilia timu
yao, nawaomba wasikate tamaa kwasababu hii ni timu yao”, anamaliza kocha
huyo wa kiganda.
Mchezo ujao wa ligi Simba itakutana na Mbeya City March 6, 2016
mchezo ambao utapigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment