Baada ya kuambulia kichapo cha 3-1 mikononi mwa Leicester City mkufunzi wa Manchester City sasa ameanza kusingizia jua.
Kocha Manuel Pellegrini anasema Leicester wanabahati ya kuendelea kupata matokeo mazuri katika ligi kuu ya Uingereza kwa sababu hawana mechi nyini na hawashiriki mashindano makubwa tofauti na wapinzani wao wakuu timu ya Arsenal.
Wachezaji wa Leicester City wakiwa wakishangilia.Vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza wamesalia na mechi 13 pekee msimu huu kwani wameshakwisha tupwa nje ya mashindano mengine.
Kwa upande wake vijana wa Pellegrini wamesalia na takriban mechi 27 katika kipindi hicho wanashiriki ligi nne tofauti kwa wakati mmoja wanawania ligi ya mabingwa barani Ulaya,ligi kuu ya Uingereza,Ligi One Cup na kombe la FA.''Bila shaka ukilinganisha mahitaji yetu na idadi ya mechi tulizoratibiwa kucheza kufikia mwisho wa msimu ni zaidi ya mara mbili ya Leicester.''
''Kwa sasa wameelekeza bidii yao yote kwenye mechi hizi za ligi na hivyo wana muda bora wa kupumzika na kujiandaa kwa mechi ijayo'' alisema Pellegrini.
Man City wameshuka hadi nafasi ya nne kufuatia kichapo hicho mikononi mwa Leicester ambao sasa wamefungua pengo la alama 5 zaidi ya washindi wa pili Tottenham.
Tunawachezaji wengi majeruhi kwa sababu tunacheza mechi zaidi ya nne kwa juma moja kwa mfano wapo wkina Vicent Kompany na Eliaquim Mangala kwenye safu ya ulinzi na kwenye mashambulizi wapo wengi zaidi Kevin De Bruyne,Jesus Navas,Wilfried Bony,Samir Nasri na David Silva wote majeruhi',alisema Pellegrin.
Kwa sasa klabu ya Manchester City wanakaribiwa na ushindani kutoka kwa Tottenham na Arsenal ambapo jumapili watacheza na Tottenham,huku timu ya Arsenal itakuwa nyumbani kumenyana na vinara wa ligi Leicester City katika uwanja wa Emirates.
No comments:
Post a Comment