KOCHA PEP GUARDIOLA KUCHUKUA MIKOBA YA MAN CITY JULAI - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday 2 February 2016

KOCHA PEP GUARDIOLA KUCHUKUA MIKOBA YA MAN CITY JULAI


Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa ataondoka Etihad mwisho wa msimu.
Pep Guardiola atakuwa meneja mpya wa Manchester City. Guardiola amesaini mkataba wa miaka mitatu Etihad.
Guardiola, atachukua majukumu hayo kuanzia Julai, klabu hiyo ya ligi ya premier imetangaza. Meneja wao wa sasa Manuel Pellegrini ataondoka klabu hiyo Juni 30 baada ya kumalizika kwa msimu wa sasa.
“Kutokana na heshima yetu kwa Manuel Pellegrini na wachezaji, klabu ingependa kufanya wazi uamuzi wake ili kuondoa nafasi ya uvumi,” City wamesema kupitia taarifa kwenye tovuti yao.

No comments:

Post a Comment