CHRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday 25 February 2016

CHRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, ameweka rekodi kwa kuwa mwanamichezo wa kwanza kuweza kufikisha wafuasi zaidi ya milioni 200 katika mitandao ya jamii.

Tovuti rasmi ya takwimu za mitandao ya ‘hookit.com’, imechapisha ripoti inayomdhihirisha Ronaldo kuwa na wafuasi milioni 109.7 Facebook, milioni 49.6 Instagram na milioni 40.7 Twitter.


Kwa mujibu wa takwimu hizo, nyota wa Barcelona Lionel Messi naye amebainishwa kufuatia wa pili kuwa na jumla ya wafuasi milioni 120.8 licha ya kutotumia mtandao wa jamii wa Twitter.lionel-messi-babyWanamichezo wengine wa mpira wa kikapu waliokuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya jamii ni kama vile LeBron James (milioni 68.7), Michael Jordan (milioni 35.4), Kobe Bryant (milioni 34.8), Kevin Durant (milioni 30) na Stephen Curry (milioni 17.6).

No comments:

Post a Comment