NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub
‘Cannavaro’ amesema anafurahia kurudi uwanjani wakati timu yake bado
ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu.
Cannavaro hajaichezea Yanga tangu Oktoba mwaka jana kutokana na maumivu ya kisigino cha mguu aliyoyapata akiwa na timu yake ya taifa ya Zanzibar katika michuano ya Chalenji iliyofanyika Ethiopia.Cannavaro amesema amefurahishwa na bidii iliyokuwa ikioneshwa na wachezaji wenzake kwa kuipigania timu yao na kuifikisha hapo ilipo na anaamini wataendelea kufanya hivyo hadi mechi ya mwisho ili kutetea ubingwa wao msimu huu.
Beki huyo ambaye hivi karibuni
alitangaza kujiuzulu kuichezea ‘Taifa Stars’, alisema hamasa aliyoikuta
ndani ya timu inamfanya kufanya kazi ya ziada ili kurudi kwenye kikosi
cha kwanza kama ilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment