Rais mstaafu JK ampongeza Samatta kwa Tuzo ya Afrika - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday, 12 January 2016

Rais mstaafu JK ampongeza Samatta kwa Tuzo ya Afrika


Samatta JK (1) Nahodha Mpya wa Taifa Stars na mshambuliaji wa TP Mazembe ya Congo, Mbwana Ally Samatta akimuonesha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani aliyoipata usiku wa kuamkia juzi Abuja, Nigeria. Hafla imefanyika leo kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar.Samatta JK (2) Kikwete (katikati) akitoa neno la kumpongeza Mbwana Samatta kwa kunyakua tuzo hiyo, Kulia ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye na kushoto ni Mbwana Samatta.samBaadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye hafla hiyo leo. samattasNyota wa Soka wa Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Kikwete, aliyokuwa akiitumia katika timu ya TP Mazeembe ya Congo DRC, katika hafla ya Kikwete iliyofanyika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili yaRais huyo mstaafu kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.Samatta JKMwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Kikwete akizungumza na kumpongeza Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta (kushoto), alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo. Kulia ni Waziri Nape.Samatta JK 3)Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa ukumbini na Nyota wa Soka Tanzania, aliyeshinda Tuzo ya mwanasoka Bora wa Afrika kwa Wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta, alipokutana na mchezaji huyo leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, kwa ajili ya kumpongeza kufuatia kutwaa tuzo hiyo.DSC_0023Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Kikwete kuzungumza na waandishi wa habari, katika hafla hiyo ya kumpongeza Samatta. Samatta JK (3) Waziri Nape Nnauye akizungumza jambo.Samatta JK (4) Wanahabari wakichukua matukio.
Samatta Kikwete (1)Kikwete na Samatta wakiongozana kutoka ndani ya Ofisi za CCM, Lumumba jijini Dar.Samatta Kikwete (2) …Akiagana na Viongozi hao.Samatta Kikwete (3)…Samatta akiondoka Ofisini hapoSamatta Kikwete (4)…Akielekea kwenye gari ili aondoke.Samatta Kikwete (5)…Akipanda kwenye gari tayari kwa kuondoka Lumumba.
RAIS wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, leo amekutana na mwanasoka Mbwana Samatta ambaye anaendelea kupokea pongezi za Watanzania kwa ushujaa wa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa wale wanaocheza soka ndani ya Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Rais  huyo mstaafu amempongeza kwa mafanikio hayo lakini akatoboa siri kuwa yote ni matokeo ya wosia aliompa walipokutana jijini Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo alimtaka awaze mafanikio ya juu zaidi hasa kucheza Ulaya badala ya kujiona kama amefika akiwa na kikosi cha TP Mazembe.
Katika mkutano na waadishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa  Lumumba jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema ana kila sababu ya kumpongeza mshambuliaji huyo ambaye anaelekea kwenda kucheza soka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji kwani ndiye mkombozi wa taifa ambalo limekuwa na ukame kwenye michezo huku akiiomba wizara  husika ya michezo kuhakikisha wanamsaidia katika kila hatua.
“Tanzania tumekosa furaha muda mrefu kwenye michezo, tumekosa makombe miaka mingi, lakini Samatta leo hii ametuinua kwa kuleta tuzo hii. Lazima tumpongeze.
“Nilikutana naye Kinshasa ambako nilimisihi sana alenge juu zaidi na sio Mazembe tu na shabaha kubwa iwe ni Ulaya ili nasi siku moja tumuone kwenye runinga akicheka na nyavu. Alitekeleza nilichomwambia na kweli timu nyingi leo hii zinamtaka huko Ulaya. Nimeomba wizara ya michezo waone jinsi ya kumsaidia katika kila hatua atakayopiga,” alisema kiongozi huyo wa zamani.
Kwa upande wa Samatta amempongeza Kikwete na serikali yake ya  awamu ya nne kwa kuwa naye bega kwa bega kwa kila hatua aliyoipiga.
Aidha Samatta alimkabidhi JK zawadi ya jezi ya TP Mazembe Na. 9 aliyokuwa akivaa klabuni hapo ambayo anaiacha baada ya kupata dili Ubelgiji anakoelekea sasa.

No comments:

Post a Comment