MATOKEO LIGI KUU BARA JANA TAREHE 16/01/2016 - TANZA MEDIA ONLINE

Sunday 17 January 2016

MATOKEO LIGI KUU BARA JANA TAREHE 16/01/2016


Mechi za Ligi Kuu Bara zilizopigwa Jumamosi zilikuwa na mvuto wa aina yake lakini mechi tatu ndiyo zilivuta wengi.

Mechi ya kwanza ni Simba ilikuwa ikipambana na Mtibwa Sugar huku ikiwa na Kocha mpya, Jackson Mayanga ambaye aliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Mechi ya pili ni kule jijini Mbeya ambako wenyeji Mbeya City waliiangusha Mwadui FC kwa bao 1-0 na mechi ya tatu; Kocha Mkuu, Abdallah ‘King’ Kibadeni anayeifundisha JKT Ruvu alipokutana na kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam
 
Mechi baina ya azama fc dhidi ya african sports ya tanga iliochezwa kwenye uwanja wa chamazi hapo jana usiku ilimalizika kwa sare ya 1-1

No comments:

Post a Comment