Kendrick Lamar kukabidhiwa ufunguo wa Compoton - TANZA MEDIA ONLINE

Sunday 17 January 2016

Kendrick Lamar kukabidhiwa ufunguo wa Compoton


Rapper Kendrick Lamar ameuwakilisha vyema mji wake wa Compton kwenye muziki na sasa mji wake umeamua kumpa heshima ya kuushika ufunguo wa mji huo.
Meya wa mji huo, Aja Brown  ametangaza kuwa K dot atakabidhiwa ufunguo wa mji huo mwezi ujao [Feb. 13] kama heshima ya kuutambulisha vyema na kuupa heshima.
Kendrick Lamar ni mmoja ya wasanii walioitangaza zaidi Compton ukiachana na wasanii wa kundi la N.W.A, Wakati ana umri wa miaka 8 alienda kushuhudia utengenezaji wa video ya 2pac Shakur na Dr.Dre “California Love”, amewahi kusema kuwa hao ni moja ya watu wenye mchango mkubwa kwenye muziki wake

No comments:

Post a Comment