Hii ndio Sababu ya Eminem kupiga chini dili la kutengeneza soundtrack ya Fast 7 ndio hii. - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday 14 January 2016

Hii ndio Sababu ya Eminem kupiga chini dili la kutengeneza soundtrack ya Fast 7 ndio hii.


Jake-Gyllenhaal
Rapa 50 Cent amesema Eminem alikuwa msanii wa kwanza kupewa mchongo wa kuitayarisha soundtrack ya filamu ya Fast 7 “See You Again” kabla ya Wiz Khalifa.
50 Cent anasema Eminem alikataa mchongo huo kutokana na kazi aliyokuwa nayo ya kutengeneza soundtrack ya filamu ya “Southpaw”.
Kwa mujibu wa 123Bored.com Eminem alifanyiwa interview na Boomer & Carton radio nakusema “Nilipewa shavu la “See You Again,” ila milikata sababu nilikuwa natayarisha soundtrack ya filamu ya Southpaw na dili lilikwenda kwa Wiz Khalifa na Charlie Puth ambao walifanya wimbo huo wa filamu ya Furious 7“.
Wimbo wa “See You Again” ni miongoni mwa nyimbo tano bora zaidi mwaka 2015 na sasa wimbo huu umetajwa kuwania tuzo za Grammy kama wimbo bora wa mwaka Wiz Khalifa Ft Charlie Puth “See You Again” > Grammy for Song Of The Year, pia umeshatazamwa na zaidi ya watu bilioni moja duniani.

No comments:

Post a Comment