LEMA AKAMATWA TENA NA POLISI - TANZA MEDIA ONLINE

Friday 27 April 2018

LEMA AKAMATWA TENA NA POLISI


 Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambapo amekamatwa na jeshi la polisi na kufunguliwa mashtaka mapya kuhusu uchochezi kutokana ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Magufuli. 
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mremaamesema kuwa Lema alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita. 
“Polisi Arusha wamemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa “uchochezi”. Dhidi ya Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota” amesema Mrema 
“Lema alihudhuria Mahakamani leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa. Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale” amesema John Mrema
 

No comments:

Post a Comment