Msanii wa muziki wa Hip Hop, Stamina ambaye kwa pamoja na Roma Mkatoliki anaunda kundi la ROSTAM amefunguka kuonyesha kushangazwa na maamuzi yaliyofanywa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza kumfungia Roma Mkatoliki.
Amesema hayo baada ya siku ya jana Roma Mkatoliki kufungiwa kujihusisha na sanaa kisa kutofanya marekebisho ya wimbo wao wa Kibamia kama alivyoagizwa na BASATA baada ya kuonekana wimbo huo una kasoro.
“Kibamia ilitoka Novemba 22, 2017 na BASATA Roma Mkatoliki tuliitwa Disemba 6, 2017 na Mhe. Waziri akasema wametupa miezi sita na leo ndio kwanza Machi 1, 2018 mbona miezi sita bado au miezi sita ya Tanzania iko tofauti na kalenda ya dunia nzima? Mna tatizo gani na wasanii wetu BASATA na Wizara? Mnakuza au mnauwa sanaa?,” Stamina alihoji kupitia instagram yake.
Stamina na Roma Mkatoliki kwa pamoja wanaunda kundi la ROSTAM ambao ndio wamiliki wa wimbo huo wa Kibamia lakini matokeo yake Roma Mkatoliki amechukuliwa adhabu peke yake kwa wimbo wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment