SIJALI KUTOITWA TIMU YA TAIFA BRAZIL - OSCAR - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday, 13 March 2018

SIJALI KUTOITWA TIMU YA TAIFA BRAZIL - OSCAR

Moja kati ya stori zinazochukua headlines kwa March 13 2018 ni pamoja na stori ya kiungo wa zamani wa Chelsea raia wa Brazil Oscer ambaye kwa sasa anacheza soka katika club ya Shanghai SIPG ya China kuhusu nafasi yake ya kucheza timu yake ya taifa ya Brazil.
Oscer leo ameulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na maamuzi yake ya kwenda kucheza soka China haoni yamehatarisha nafasi yake ya kuitwa katika kikosi cha timu yake ya Brazil kitakachoshiriki Kombe la dunia 2018 nchini Urusi?
“Sijali kama nitaitwa kwenda kucheza Kombe la dunia au nisipoitwa maana sitaki kubaki masikini nitakapo zeeka halafu nibaki katika kumbukumbu kuwa niliwahi kucheza Kombe la dunia”Oscer
Oscer aliamua kuondoka Chelsea mwaka 2016 na kwenda kujiunga na Shanghai SIPGya China na kuingia katika list ya wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani, hiyo ni baada ya kudumu Chelsea kwa miaka minne pekee, hivyo kwenda kwake kuchezaChina ni kwa sababu ya pesa.

No comments:

Post a Comment