MWANDISHI ANSBERT NGURUMO AKIMBIA ‘WAUAJI’, APEWA HIFADHI FINLAND - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday, 15 March 2018

MWANDISHI ANSBERT NGURUMO AKIMBIA ‘WAUAJI’, APEWA HIFADHI FINLAND


                  Mwandishi Ansbert Ngurumo.
MWANAHABARI Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi kwa muda baada ya kudai amewakimbia aliowaita “wauaji” wake.

Ngurumo amethibitisha kuikimbia Tanzania ili kulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.
“Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai, ili kunusuru uhai wangu, nililazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako nimepewa hifadhi,” alisema Ngurumo.

Aliongeza kwamba hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni “hifadhi ya kimataifa,” kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.

Aidha, vyombo vya habari vya Finland na mitandao ya kijamii, vimeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.
“Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa,” amesema Ngurumo.

SOURCE:GLOBALPUBLISHER

No comments:

Post a Comment