KATIBU
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelipongeza Baraza la Maaskofu
la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kutoa waraka
mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka.
Waraka huo ulitolewa mwishoni wa wiki iliyopita ambao mbali na
kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha
kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi
wake.”
Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu
Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali
ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo
suala la Katiba Mpya.
Akizungumza leo Machi 26, 2018 jijini Dar es salaam wakati akisoma
maazimio manne ya Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyokutana
leo, Maalim Seif amesema anafarijika kuona viongozi wa dini wanakemea
mambo ambayo hayaendi sawa nchini.
“Nimefarijika kuona viongozi wa taasisi za dini wakizungumza pale
ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Tusitafsiri kwamba wanafanya siasa,
hapana ni haki yao kukemea, ” amesema Maalim Seif.Amesema angetamani kuona viongozi wengine wa dini wakionyesha misimamo kama maaskofu hao.
Aidha, Maalim seif amemponda Mwenyekiti wa Chama hicho, Prof. Ibrahim
Lipumba kwa kitendo cha kuwavua uanachama wanachama nane na kupoteza
sifa za kuwa wabunge jambo ambalo wamepambana hadi kurudishiwa uanachama
baada ya kudai haki yao mahakamani.
Maalim amesema kwa sasa wanafanya jitihada za kisheria ili
kuwarudisha wabunge hao Bungeni wakati kesi yao ya msingi ikiwa
inaendelea mahakamani.
No comments:
Post a Comment