Wafungwa wadhibiti wa gereza Brazil - TANZA MEDIA ONLINE

Monday, 19 February 2018

Wafungwa wadhibiti wa gereza Brazil


Wafungwa wachukua udhibiti wa gereza mjini Rio de JaneiroHaki miliki ya picha
Image captionWafungwa wachukua udhibiti wa gereza mjini Rio de Janeiro
Wafungwa wamechukua udhibiti wa gereza kwenye mji wa Rio de Janeiro nchini Brazil na wanawashika mateka baadhi ya wafanyakazi wa gereza hilo.
Aidha Polisi waliojihami wanalizunguka gereza hilo lenye msongamano wa wafungwa la Japari ambalo liko chini ya udhibiti wa genge moja la wahalifu lenye guvu nyingi mjini humo.
Lakini pia Wafungwa watatu ambao walihusika katika kulidhibiti gereza hilo wamepigwa risasi lakini hawajapa majeraha ya kuwatishia maisha.
Ghasia hizo zinatokea siku mbili baada ya Rais wa Brazil Michel Temer, kusaini sheria ya kuwapa wanajeshi ruhusa ya kusimamia usalama wa mji wa Rio de Janeiro.
Maafisa wa gereza wanasema ghasia hizo huenda zimechangiwa na hatua mpya za ulinzi.

No comments:

Post a Comment