Serikali ya Mfalme Salman ya Saudi Arabia imewafuata makamanda wa vyeo vya juu jeshini akiwemo mkuu wa majeshi.Mfalme Salman pia amefanya mabadiliko kwa makanda wa vikosi vya nchi kavu na vile vya angani.
Taarifa hizo zilichapishwa na shirika rasmi la habari la Saudi Arabia la SPA, lakini hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kwa makamanda hao.
Mabadiliko hayo yanakuja wakati vita nchini Yemen, ambapo muungano unao ongozwa na Saudi Arabia unaopigana na waasi unaelekea kumaliza mwaka wake wa tatu.
Mrithi wa ufalame Mohammed bin Salman, ambaye pia ni waziri wa ulinzi anaaminiwa kuhusika kwenye mabadiliko hayo.
Mwaka uliopita watu mashuhuri nchini Saudi Arabia wakiwemo wana wafalme, mawaziri na wafanyabiashara matajiri walifungiwa kwenye hoteli ya kifahari ya Ritz-Carlto, wakata mwana mfalme huyo aliongoza mikakati dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.
No comments:
Post a Comment